Alhamisi ya leo kupitia Clouds Fm kwenye Leo Tena, Hekaheka inahusu mama ambaye amefiwa na mtoto wake akiwa mikononi mwa Polisi, ambapo alikamatwa wakati mtoto wake akiwa anaumwa.
Kisa cha mama huyo kukamatwa ni hali ya kutokuelewana baina yake na Kijumbe ambaye anakusanya hela ya mchezo, ambapo mama huyo alikwenda kwa Kijumbe kudai hela yake ya mchezo, Kijumbe alimwambia hakuwa amekusanya hela hizo hali iliyopelekea waanze kushambuliana kwa maneno
Baada ya kupishana baina yao, Kijumbe alikwenda kuripoti kituo cha Polisi kwamba amefanyiwa fujo na mama huyo, ambapo alikamatwa na kuwekwa ndani pamoja na mtoto wake ambaye.
Jitihada za mume wake na mama yake mzazi kuomba kumchukua mtoto wakampe dawa hazikufanikiwa na saa tisa usiku mtoto huyo akafariki na baadaye Polisi wakamwachilia mama huyo huru.
Kijumbe aliyempeleka mama huyo kituoni anashikiliwa na Polisi.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Je Umezisoma Hizi?
- Utata wa picha za utupu za msichana huyu kwenye mitandao sasa zamtokea puani26 Mar 20150
Kama ni mpenzi wa Hekaheka nakusogezea hii iliyosikika leo mtu wangu, inatoka Shinyanga ambapo k...Read more ?
- Ukatili: Hekaheka ya leo, mama alimmwagia mtoto wake maji ya moto04 Feb 20150
Nimekuwekea Hekaheka ya leo February 04, inatokea Buguruni Dar inahusu mama ambaye amekuwa na ta...Read more ?
- Hekaheka ya leo inamhusu msichana aliyepelekwa Oman kufanya kazi za ndani.19 Jan 20151
Kwenye Hekaheka ya leo Jan 19 inatokea Dar inamhusu Binti mmoja aliyepelekwa Oman na mtu aliyemf...Read more ?
- Hekaheka, Inahusu mwanaume aliyechoma moto nguo za mke wake na watoto13 Jan 20150
Kama ulipitwa na Hekaheka ya leo January 13 inatokea maeneo ya Kimara Dar, inahusu mw...Read more ?
- Hekaheka ya leo, Inamhusu Mama anayejisaidia kwenye ndoo! story iko hapa08 Jan 20150
Hekaheka ya leo Jan8, inatokea huko Shinyanga, ambapo watu wanaishi nyumba moja wamemla...Read more ?
- Hekaheka Nesi Aliruhusu Mtoto Aliyezaliwa Kuzikwa Kumbe Alikuwa Hai..Story iko hapa06 Jan 20150
Mama mmoja mjamzito alikwenda Hospitali ya Mkoa Morogoro siku ya jana, alipofika hospitali hapo ha...Read more ?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
Post a Comment