
Nimekuwekea Hekaheka ya leo February 04, inatokea Buguruni Dar inahusu mama ambaye amekuwa na tabia ya kumtesa mtoto wake wa kiume kwa kumchoma na maji ya moto kitendo kilichofanya majirani kushikwa na hasira na kuamua kumsaidia kijana huyo kwa kumpeleka Polisi akatoe taarifa.
Majirani hao wamesema kijana mmoja alipigiwa simu na rafiki yake ambaye alimwagiwa maji ya moto saa tisa usiku na mama yake, wakampeleka Polisi na kupewa PF3 ya matibabu.
Kijana huyo amesema kuwa mama yake alimgongea mlango usiku na kumuuliza alikoweka pasi, akajibu kwamba hajaiona na kuondoka baadaye alimgongea tena na alipofungua alimwagia maji ya moto na kumtoa nje, halafu akafunga mlango.
Mjumbe ambaye amejitolea kukaa na kijana huyo amesema kuwa sio mara ya kwanza mama huyo kufanya tukio kama hilo, alishawahi kuwatibu watoto wake wawili majeraha ya moto ambao walienda nyumbani kwake baada ya kuwachoma na mama yao, kwa sasa mama huyo anashikiliwa kituo cha Polisi.
Bonyeza play kusikiliza Hekaheka ya leo hapa.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment