
Wakati huo ilikuwa usiku, umeme ulikuwa umekatika na wakalazimika kutumia tochi ya kwenye simu wakati akijifungua.
Nesi huyo alikuja kumpa msaada baadaye akamwambia kwamba tayari mtoto wake ameshafariki, hivyo awaite ndugu zake ili wamchukue mtoto huyo wakazike.
Ndugu walimchukua mtoto huyo akiwa amewekwa ndani ya ndoo, walipofika nyumbani waligundua kwamba mtoto alikuwa mzima bado lakini waliporudi tena Hospitali jitihada za kumtibu hazikusaidia kwani alifariki wakati wakianza jitihada za kumshughulikia.
Mganga Mkuu Hospitali ya Mkoa Morogoro amesema kuwa hakuwepo kwa kuwa yupo likizo.
Isikilize hapa Hekaheka yote kwa kubonyeza play.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment