Hekaheka ya leo Jan8, inatokea huko Shinyanga, ambapo watu wanaishi nyumba moja wamemlalamikia mpangaji mwenzao kwa kitendo chake cha kutokwenda chooni na kujisaidia kwenye mifuko na kutupa hovyo uchafu huo wakati wa usiku, baada ya kumlalamikia aliamua kutumia ndoo kujisaidia kwa madai kuwa hawezi kwenda chooni kwa kuogopa ugonjwa wa UTI.
Mwanamke huyo alipoulizwa alisema huwa anajisaidia nyumba ya jirani kwa rafiki yake kutokana na choo chao kujaa, amekataa kwamba huwa anajisaidia kwenye ndoo, amesema amekuwa akiogea ndani kwake pamoja na kufua na kisha kumwaga maji nje kitendo kinachowafanya wafikirie kuwa anajisaidia kwenye ndoo.
Isikilize hapa Hekaheka yote kwa kubonyeza play
Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi
Post a Comment
Post a Comment