Uuzaji wa bangi kama ulevi wa starehe utaanza kuuzwa rasmi hii leo
katika jimbo la Marekani la Washington. Hili ni jimbo la pili nchini
humo kuhalalisha bangi kwa matumizi ya burudani, baada ya jimbo la
Colorado kufanya hivyo. Mapato ya kodi
kutokana na uuzaji wa bangi katika jimbo la Colorado yamefikia dola
milioni kadhaa sasa. Mchakato huo utadhibitiwa kwa makini katika jimbo
la Washington. Maduka ishirini na tano tu ndio yamepata leseni ya kuuza
mpaka sasa, ingawa maafisa wanasema idadi hiyo huenda ikaongezeka na
kufikia maduka takriban mia moja.
Majimbo mengine 23 nchini Marekani
tayari yanaruhusu uuzaji na ununuaji wa bangi lakini kwa sababu za
kitabibu.
UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WHATSAPP 0712-483 331
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu BONYEZA HAPA
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment