Tukio
hilo lilitokea Jumamosi iliyopita mnamo saa 11:00. Mwanamke huyo alidai
kuwa kabla ya kujeruhiwa aliitwa na jirani huyo na bila kujua
alichoitiwa, alikwenda nyumbani kwa mwanamke huyo ambako alifungiwa
ndani.
Alisema akiwa ndani jirani huyo alimtuhumu kufanya mapenzi na mume wake na hata alipojaribu kukataa, alitishia kumuua.
“Kwa
kuhofia kuuawa niliona nikubali tuhuma hizo na aliniuliza ni mara ngapi
nilifanya mapenzi na mume wake na kama nilikuwa napewa pesa, hivyo
nilikiri kufanya mapenzi mara mbili na kwa mara ya kwanza alinipa
Sh2,000 na mara ya pili alinipa Sh5, 000 na baada ya hapo aliniachia na
nikarudi nyumbani,” alidai Rehema.
Rehema
aliendelea kudai kuwa siku hiyo mnamo saa 11:00 jioni binti wa mwanamke
huyo alifika tena nyumbani kwake na kumwambia anaitwa tena na mama
yake.
Naye
bila ya hofu alikwenda nyumbani kwa mwanamke huyo na alipofika
aliingizwa kwenye chumba kimoja ambacho alikuwamo mume wa mwanamke huyo
na kuanza kumpiga, akamvua nguo na kumkatakata kwa kiwembe shavuni na
mikononi.
Alidai
kuwa baadaye mwanamke huyo alianza kumpiga mume wake, lakini mwanaume
huyo alichomoka na kukimbia na alipomkimbiza ndipo yeye alipopata nafasi
ya kutoka nje akiwa amebaki hana nguo huku akichuruzika damu.
Aliporudi
nyumbani kwake, Rehema alisema aliongozana na mume wake Godfray
Shichonge na ndugu zake wengine kwenda polisi kutoa taarifa na baadaye
walipewa PF3 kwenda kutibiwa.
Godfray
Shichonge, ambaye ni mume wa Rehema alidai kuwa tangu alipoanza kuishi
na mkewe hajawahi kusikia taarifa zozote za kufanya mapenzi nje ya ndoa
yao na kuwa katika mtaa huo ni wageni na hawana mazoea na mtu yeyote.
“Alipoitwa
nyumbani kwa mama huyu na kufanyiwa ukatili aliniacha nyumbani nikiwa
nimepumzika na kabla ya kuondoka aliniaga na nikadhani kuwa ni masuala
ya kawaida ya kina mama.
Ghafla
nilishtuka usingizini kutokana na kilio cha mke wangu aliyerudishwa
nyumbani akiwa anavuja damu na akiwa amevuliwa nguo zote,” alisema
Shichonge.
Alisema
kitendo alichofanyiwa mke wake ni udhalilishaji kwani hata kama
mwanamke huyo alikuwa akimtuhumu kufanya mapenzi na mume wake alipaswa
kufuata sheria na siyo kumjeruhi kwa kumkata kwa viwembe na kumvua nguo.
Mjumbe
wa mtaa huo, Dimoso Frances alisema baada ya mwanamke huyo kumkatakata
mwenzake kwa viwembe, alikwenda nyumbani kwa mjumbe huyo na kuomba
asamehewe kwani alifanya hivyo kutokana na hasira.
Dimoso
alidai kuwa kutokana na hali ya majeruhi kuwa mbaya, hakuweza kutoa
uamuzi wowote na hivyo aliamua kufuatilia taarifa hizo polisi ambako
aliambiwa kuwa tayari kesi ya kujeruhi ilishafunguliwa kwa jalada namba
MORO/IR/4009/2014.
Kamanda
wa polisi wa Mkoa wa Morogoro, Leonard Paulo alikiri kutokea kwa tukio
hilo na kusema kuwa tayari kesi ilishafunguliwa na mtuhumiwa amekamatwa
akiendelea kuhojiwa zaidi.
Kamanda Paulo alisema baada ya mahojiano hayo na uchunguzi utakapokamilika, mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani.
via>>mwananchi
UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WHATSAPP 0712-483 331
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu BONYEZA HAPA
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment