Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Msichana aliyejeruhiwa na msanii Abdulmalick Ahmed ‘Ben’.

MSANII wa filamu za Kibongo, Abdulmalick Ahmed ‘Ben’ anasakwa na jeshi la polisi akidaiwa kumjeruhi mzazi mwenziye, Leyla Abdalah, mkazi wa Magomeni-Mikumi, Dar.Akizungumzia tukio hilo, Leyla alisema mwigizaji huyo ambaye pia hufahamika kwa jina la Serengo amekuwa akimfanyia fujo mara kwa mara kwani Januari, mwaka huu, akiwa katika Ukumbi wa Travertine, Magomeni, Dar, alikutana na msanii huyo ambaye alimlazimisha waondoke pamoja, alipokataa akaanzisha vurugu.
 
Leyla alisema kwa kuwa msanii huyo walishamwagana kwa talaka tatu miaka mitatu iliyopita, alikataa kuondoka na mzazi mwenziye huyo na kudai mbali na kuachana naye, alikuwa na mpenzi wake mpya.
 
“Nilimuambia siwezi kwenda naye popote, alinivamia na kuanza kunishushia kipigo kikali na kunichania nguo mbele za watu, wadau walijaribu kugombelezea sikujisikia poa ndipo nikakimbizwa Hopitali ya Magomeni, Dar nikalazwa wodi ya mapumziko, nikatoka,” alisema Leyla na kuongeza:
 
“Nikiwa katika maumivu ya kipigo hicho, Jumamosi iliyopita Ben alinishushia tena kipigo cha mbwa mwizi baada ya kukutana naye kwenye Baa ya Kilimanjaro, Magomeni-Mapipa.

 
Abdulmalick Ahmed ‘Ben’.

“Anilikuta na wenzangu, akanivamia tena na kuniambia anataka tuondoke, nilipomuuliza twende wapi, akanijibu kwa ukali weee twende tu, nikamkatalia, akapanda juu ya meza na kunijeruhi kichwani na kiti ndipo nikaona bora nikimbilie Kituo cha Polisi cha Magomeni.
 
“Nilimfungulia kesi kwenye jalada lenye namba MG/RB/1234/14 SHAMBULIO LA KUDHURU MWILI,” alisema Leyla. Gazeti hili lilimtafuta Ben nakumsomea madai ya mzazi mwenzake huyo ambapo alikiri kuzaa naye na kudai migogoro hiyo inasababishwa na yeye kudai mtoto wake.
 
“Huyo mwanamke ni kweli nilizaa naye lakini kwa sasa sina haja naye hata kiduchu, nina mwanamke yuko bomba ile kinoma ukimuona mwenyewe utabloo, siwezi kurudia matapishi.
 
“Huyo anataka kuniharibia tu, kila nikimfuata anipe mtoto wangu anajifanya mpana na kuniletea ndivyo sivyo ndiyo maana tunakwaruzana mara kwa mara,” alisema Ben.
GPL

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top