KLABU
za Yanga na Simba zimeagizwa kulipa jumla ya sh. Milioni 25 kutokana na
uharibifu wa viti na vurugu zilizofanywa na washabiki wao kwenye mechi
ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Yanga na Al Ahly ya Misri iliyochezwa
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.Yanga
italipa sh. milioni 15 ambayo ni gharama ya uharibifu wa viti
uliofanywa na washabiki kwenye mechi hiyo. Pia imepigwa faini ya sh.
milioni tano kutokana na vurugu za washabiki wake. Nayo Simba imepigwa
faini ya sh. milioni tano kutokana na washabiki wake kuhusika katika
vurugu hizo.
Uamuzi huo umefanywa na Kamati ya
Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) katika kikao
chake cha dharura kilichofanyika jana (Machi 19 mwaka huu) jijini Dar es
Salaam.
TFF imetoa onyo kwa washabiki wa mpira wa
miguu kujiepusha na vurugu viwanjani ikiwemo uharibifu wa miundombinu
mbalimbali ya viwanja ikiwepo viti, na imeahidi kuchukua hatua kali
zaidi kwa klabu na washabiki wake iwapo vitendo hivyo vitajitokeza tena.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment