Staa Ray C
almaarufu "Kiuno Bila Mfupa" akielekea kwenye gari lake mara baada ya
kupata dozi yake ya dawa ya kuondoa sumu ya madawa ya kulevya
Kikosi Kazi cha Global Publishers, kimefanikisha zoezi la kumnasa laivu Mbongo-Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’, akizama na kuchukua dozi ya dawa za kuondoa sumu ya madawa ya kulevya ‘unga’ mwilini, Amani lina tukio kamili.
Kazi
hiyo nyingine nzuri kwa OFM ilifanyika juzi (Jumanne), majira ya saa
3:30 asubuhi ndani ya Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar ambapo staa
huyo almaarufu Kiuno Bila Mfupa alifika eneo hilo kwa ajili ya kuchukua
dozi hiyo ya dawa aina ya Methadone.
Awali, miezi miwili iliyopita, Amani
lilidokezwa kuwa Ray C amekuwa akionekana hospitalini hapo hivyo kachero
wa OFM kutakiwa kuthibitisha juu ya habari hiyo.
Kachero huyo alianza kumfuatilia staa
huyo wa Wimbo wa Na Wewe Milele hatua kwa hatua lakini kila
alipomvizia ilishindikana kumnasa hadi juzi, alipojaa kwenye kumi na
nane.
Kilichofanyika ni kwamba kamanda huyo
wa OFM aliamua kumkeshea maeneo hayo na hatimaye akambamba kilaini
akizama ndani ya hospitali hiyo.
RAY C LAIVU
Ray
C alionekana laivu akiingia hospitalini hapo akiendesha gari aina ya
Toyota Carina, majira hayo ya saa 3:30 asubuhi na akatoka saa 4:30
asubuhi ambapo muda wa kuingia na kutoka kamanda wetu alikuwa
akimfuatilia kwa kuchukua picha za matukio yote hadi alipoondoka kwenye
eneo la hospitali hiyo.
Ray C akikatiza geti la Hospitali ya Mwananyamala baada ya kuchukua dozi.
Uchunguzi wa OFM hospitalini hapo ulibaini
kwamba mwanadada huyo aliyepanga kurudi stejini muda wowote kuanzia
sasa, alipofika alikwenda moja kwa moja kwenye chumba maalum cha daktari
ambapo alikabidhiwa dozi hiyo ya Methadone na ushauri nasaha.
BOFYA HAPA KUMSIKIA KIUNO BILA MFUPA
OFM haikutaka kukamilisha kazi hiyo
bila kusikia kauli ya mrembo huyo, hivyo ilimtafuta ili aweze
kuzungumzia juu ya uchukuaji wa dozi hiyo tangu alipotangaza kuachana na
madawa ya kulevya kwa msaada wa Rais wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho
Kikwete.
Alifunguka: “Ni kweli nina kawaida ya
kwenda kuchukua dawa kila siku asubuhi kwenye Hospitali ya
Mwananyamala, Dar maana ndicho kituo nilichopangiwa tangu nilipoachana
na utumiaji wa madawa za kulevya.
“Kwa sasa hali yangu iko safi yaani naweza kusema nimeshapona moja kwa moja isipokuwa nakamilisha dozi yangu tu.
“Pia nipo kwenye mpango wa kuanza
kuzunguka karibu Tanzania nzima ili niweze kutoa elimu kwa waathirika
wengine wa madawa ya kulevya.
“Kuhusu mpango huo, tayari
nimeshafungua ofisi kwa ajili ya kusimamia Foundation (taasisi) hiyo na
nimetoa fursa kwa Watanzania waweze kunitumia nembo au logo nzuri na
atakayeshinda mwisho wa mwezi huu atapata shilingi laki tano kama
zawadi.
“Nafarijika sana na watu wote
walionipigania hadi leo ninajitambua kama hivi, ingawa kuna watu wengi
sana walikuwa hawaamini juu yangu kama kweli ningeweza kuachana na
utumiaji wa dawa za kulevya hadi kufikia kiasi hiki, hivyo basi
mizunguko yangu ya kuelimisha watu hawa itakuwa kama moja ya fadhila
yangu kwa Mungu na wote walionipigania kwa hili.”
MADAI YA KURUDIA UNGA
“Hilo siyo kweli kwa sababu kwanza
nitaharibu dozi na pia madaktari wangejua. Siwezi kurudia kwani najua
mateso niliyokutana nayo na pia watu walivyonipigani uhai wangu,”
alisema staa huyo mkubwa.
DAKTARI ANASEMAJE?
Ili kuthibisha kama amerudia au la,
OFM ilizungumza na mmoja wa madaktari wanaomhudumia Kiuno Bila Mfupa kwa
sharti la kutotajwa ambaye alithibitisha kuwa kwa sasa Ray C hatumii
unga kwani wangemshtukia.
>>>>GPL
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment