Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Wachezaji wa Yanga wakishangilia bao lililofungwa na Didier Kavumbagu (wa pili kulia), wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara ilipopambana na Azam  FC kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo (jana). Timu hizo zilitoka sare ya 1-1. bao la Didier Kavumbagu (wa pili kulia) lililopelekea mauti ya Deodatus Lusinde.
 
SHABIKI wa Timu ya Yanga SC, Deodatus Isaya Lusinde, mkazi wa Kipunguni A, amefariki dunia leo (jana) baada ya kuanguka ghafla wakati akishangilia bao la Yanga lililofungwa na Didier Kavumbagu katika dakika ya 14 kipindi cha kwanza.
Marehemu amepoteza maisha akiwa chumba cha matibabu mara baada ya kuwekewa mashine ya oksijeni na taarifa kuhusu kifo cha shabiki huyo zimethibitishwa na mmoja wa madaktari aliyemhudumia akiwa uwanjani kabla ya mauti kumfika, Nassor Matuzya. 
Bwana Isaya alikuwa Meneja wa Bar ya Rose Hill iliyopo Segerea jijini Dar. Ameacha mke aitwaye, Rose William Lusinde ambaye ni askari magereza.
 
Marehemu amekutwa na mauti hayo wakati wa mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara, kati ya timu yake ya Yanga na Azam, mchezo uliomalizika kwa sare  ya bao 1-1.
 
Mungu ailaze roho ya mwanamichezo, Deodatus Isaya Lusinde mahali pema peponi. AMEN!

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top