Timu ya Yanga na Mbeya City zimekutana leo katika raundi ya pili ya ligi ya vodacom na yanga kuitandika magoli 3 kwa 1.
Mabao ya Yanga yamefungwa na Kpah Sherman, Salum Telela na Nadir Haroub ‘Cannavaro’.
Bao la kufutia machozi la Mbeya City limefungwa na Themi Felix ‘Mnyama’.
Kwa matokeo haya, Yanga wameendelea kuwa wababe dhidi ya timu inayomilikiwa na halmashauri ya jiji la Mbeya.
Matokeo ya leo yanawafanya Yanga wazidi kupaa zaidi kileleni wakijikusanyia pointi 46 baada ya kucheza mechi 21.
Nafasi ya pili inashikiliwa na mabingwa watetezi Azam fc wenye pointi 38 kufuatia kushuka dimbani mara 20 na hapo jana walitoka sare ya 1-1 dhidi ya Mtibwa Sugar uwanja wa Manungu, Turiani, Mkoani Morogoro.
Matokeo mengine stend United imeifunga Polisi Morogoro goli moja bao pekee la Mnigeria, Abasirim Chidiebele limewapa Stand United pointi tatu katika mechi ya ligi kuu soka Tanzania bara dhidi ya Polisi Morogoro iliyopigwa uwanja wa CCM Kambarage jioni ya leo.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment