Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Mayasa Mariwata na Shani Ramadhani
Mwanamke mmoja anayekadiriwa kuwa na miaka 35 amekutwa porini akiwa uchi wa mnyama na hawezi kuongea hali iliyozua hofu kwa wananchi na kudai ni msukule.
 
Tukio hilo lilijiri hivi karibuni maeneo ya Pugu Mnadani, wilayani Ilala jirani kabisa na Pori la Hifadhi ya Kisarawe mkoani Pwani. Baadhi ya wakazi walimhusisha mwanamke huyo na imani ya msukule wakidai huenda alitoroka kutoka kwenye makazi yake kabla ya kukatwa ulimi.
 
Akizungumza na gazeti hili, shuhuda mmoja wa tukio hilo, Said alisema baada ya kumkuta katika hali hiyo walianza kwa kumsitiri kwa nguo kisha mwanamke mmoja mganga alimlisha dawa ya kienyeji ndipo akaanza kuzungumza lakini kwa shida.

“Tulimuuliza jina lake akasema anaitwa Tumsifu Yesu. Alidai ameishi kwenye pori hilo kwa kipindi kirefu bila kujua alifikaje kwa vile kwao ni Iringa. “Cha kustaajabisha zaidi pale alipopewa chakula alifanikiwa kula maandazi arobaini na maji lita tano ndani ya dakika kumi tu,” alisema shuhuda huyo.
 
Akaendelea: “Baada ya kumaliza kula alionesha ishara ya msalaba kwa kumshukuru Mungu. Ndipo akapelekwa serikali ya mtaa na baadaye Kituo cha Polisi cha Pugu kwa msaada zaidi,” kilisema chanzo hicho.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro
11 Apr 2014

Post a Comment

 
Top