Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Klabu ya Juventus wamekamilisha usajili wa mshambuliaji wa Argentina, Gonzalo Higuain kutoka klabu ya Napoli kwa pauni milioni 75.5
article-3710420-36A1E3AD00000578-383_964x390
Mchezaji huyo mwenye miaka 28 amesaini mkataba wa miaka mitano baada ya Juventus kukubali kutoa kitita hicho kinachokaribia Euro milioni 90 ambazo watazilipa kwa awamu.
Malipo hayo ya Higuain aliyeanzia uchezaji wake wa kulipwa katika timu ya River Plate ya Argentina yanachukua nafasi ya tatu kwa ukubwa baada ya yale yaliyolipwa na Real Madrid walipomnunua Cristiano Ronaldo kwa Pauni milioni 80 na Gareth Bale kwa Pauni milioni 85.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro
28 Jul 2016

Post a Comment

 
Top