WATU 18 wamepoteza maisha papo hapo kwa kuteketea na moto huku wengine 11 wakijeruhiwa vibaya baada ya Basi la kampuni ya Nganga kugongana uso kwa uso na gari la mizigo aina ya Mistubishi Fuso mkoani Morogoro.
Ajali hiyo imetokea leo majira ya saa mbili asubuhi katika Kijiji cha Msimba, tarafa ya Mikumi, Wilayani Kilosa mkoani Morogoro ikilihusisha basi hilo lenye namba T373 DAH na Fuso hilo lenye namba T164 BKG.
Kamanda wa Polisi mkoani Morogoro Leonald Paulo amesema chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa Basi la Nganga kuendesha gari kwa mwendo kasi na kulipita gari lillilo mbele yake bila kuchukua tahadhari na kusababisha ajali hiyo.
Amesema basi hilo lililokuwa likitoka Dar-es-salaam kwenda Mbeya lilikuwa limepakia pikipiki katika buti, ambayo ilikuwa na mafuta hivyo baada ya kugongana palitokea mlipuko na kusababisha moto mkubwa ulioteketeza basi na lori hilo.
Kamanda Paulo amesema waliokufa ni madereva wa magari yote mawili walioteketea kabisa na moto huo na abiria walioshindwa kujiokoa, na majeruhi takribani 11 wamekimbizwa katika Hospitali ya Mtakatifu Kizzito Mikumi.
Mungu azilaze roho za marehemu mahali Pema peponi.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment