Ujumbe kwa Bi Dada (Mke, Mpenzi,
Mchepuko...)Kombe la Dunia ndiyo limefika, tungependa kufafanua na
kuweka sawa mambo kadhaa ili usiulize swali la kijinga Tanzania
haikufuzu kucheza Kombe la Dunia.
Ipo tofauti ya saa 5 kati ya Rio De Janeiro na Afrika Mashariki.
Ronaldo wa Brazil na Ronaldo wa Ureno hawana undugu.
Hakutakuwepo na mazungumzo yasiyohusu soka wakati wa kipindi cha kawaida ama ziada cha mechi na hasa wakati wa penati.
Utazishabikia
timu nitakazokuwa nazishabikia tu! Utatabasamu pale tu timu
ninayoishabikia itakapokuwa inashinda na utashangilia "goliiiiii" wakati
goli kweli limetinga nyavuni.
Wataarifu marafiki zako wasifunge ndoa, wasizae, wasiugue wala wasife katika kipindi cha Kombe la Dunia! Hatutahudhuria hayo!
Hili
ni Kombe la Dunia! Hakuna Asenali, ManU wala Barcelona. Huwa linachezwa
mara moja kila baada ya miaka minne, kwa hiyo usiniulize kama ni mechi
sawa na zilizochezwa wiki zilizopita.
Tutatizama
soap, reality show, romantic, African na sinema za Kiafrika alimradi tu
ziwe zimerekodiwa Brazil na wahusika ni wachezaji kutoka kwenye timu
zinazoshiriki Kombe la Dunia.
Ni marufuku kusifia muonekano wa Cristiano Ronaldo. Kinachomhusu hapa ni soka tu!
Kama umepitwa wakati wa kutambulishwa majina ya wachezaji, tafadhali usiniulize, "yule ni nani?"
Unapaswa
kusoma sheria za soka kabla ya kuanza kutizama Kombe la Dunia. Maswali
kama, "Mbona au Ni nani yule jamaa anakimbia karibu ya kiwanja akipepea
kibendera?" hayatavumiliwa.
Kwa
kipindi kizima cha Kombe la Dunia, rimoti itakaa kwenye mfuko wangu na
itatumiwa na mimi tu ama kwa ruhusa ya maandishi kutoka kwangu.
Nadhani tumeelewana.
Asante. Baba mwenye nyumba! BONYEZA HAPA
Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi
Post a Comment
Post a Comment