Video vixen Agnes Gerald a.k.a Agnes Masogange amefunguka kuhusu matatizo aliyoyapata mwaka jana baada ya kukamatwa uwanja wa ndege wa Or-Tambo, Afrika Kusini (July 5 2013) na mzigo uliosemekana kuwa ni dawa za kulevya. Agnes ni miongoni mwa Watanzania waliokwenda Durban, Afrika Kusini kumsupport Diamond Platnumz katika Tuzo za MTV (MAMA) weekend iliyopita, na Bongo5 ambayo pia ilihudhuria Tuzo hizo ilipata nafasi ya kufanya nae Exclusive Interview. “Ilikuwa ndio mara yangu ya kwanza kuingia jela sijawahi kuingia jela tangu nizaliwe, nilivyoingia mle ndani nikawa naomba kila siku eh Mungu wangu,” alisema Aggy.
Pamoja na mengine, Masogange ambaye kwa sasa amehamishia makazi yake jijini Johannesburg, aliweza kushare na sisi jinsi maisha yake ya jela yalivyokuwa baada ya kukamatwa na kuwekwa ndani huko Afrika Kusini. “Nilivyofika pale na watu walivyokuwa wanachukulia yani na mimi nilikuwa nahisi labda siwezi kutoka leo wala kesho, nilikuwa nahisi labda ntapigwa sentence ya miaka kumi miaka kumi na tano lakini Mungu ni mkubwa nimetoka.” Alisema. Agnes amesema kuwa kuna baadhi ya marafiki zake ambao walikuwa wanatamani afungwe: “Yah kuna wengine hadi marafiki zangu walikuwa wanapenda mi nikae ndani, si unajua sisi yani hatupendani mimi naweza nikakupenda wewe ukiwa na kitu lakini mimi nikipungukiwa kitu flani huwezi kuwa rafiki yangu tena sababu unajua Agnes kakwama kitu flani, kwahiyo atakuwaje rafiki yangu. Au wengine wanaweza kuongea ooh Agnes alikuwa anaringa sijui hivi na hivi bora ameenda jela.” Alichojifunza Jela: “Nimejifunza vingi sana sababu kule ndani sio kuzuri kabisa [kicheko] lakini naona jela ya huku (South Africa) na Tanzania ziko tofauti, jela ya huku kidogo unakula vizuri unalala vizuri baada ya siku mbili mnabadilishiwa mashuka mnapewa sabuni kila kitu, maji ya moto mnaoga [sigh] sijui kama bongo kuna maji ya moto [sigh]. Lakini mi nahisi jela ni jela unajua mtu hata uwe unakaa jela nzuri ukikosa ule uhuru tu ndio hivyo.’
Masogange pia alizungumzia ukweli wa kilichotokea hadi kukamatwa na kuwekwa ndani:
“…Watu walikuwa wanaongea ile ni drugs lakini sio drugs…, we hujui wanatengenezea nini mahospitli , zinatumika mahospitali, zinatengeneza panadol, “ Ushauri kwa wasichana wengine wanaotumiwa katika biashara ya dawa za kulevya:
Mimi nilikuwa nawashauri yani hizi kazi sio nzuri ni bora mtu utafute pesa kwa biashara nyingine lakini sio mambo ya madawa au kubebeshwa madawa ya kulevya, kwasababu yani ukishashikwa tu miaka yako ni mingi sana.
PLAY HAPA CHINI
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment