Baada ya kusambaa kwa picha ambazo si nzuri katika mazingira ya
kawaida zikimuonyesha Mhe. Kaptein Komba akiwa amepiga picha na msichana
chumban huku zikimuonyesha msichana huyo amevaa kanga na wakati
mwingine bila kuwa na nguo.
Kuzungumzia tukio hilo moja kwa moja kutoka Dodoma Mhe. Komba anasema
hajui kuhusiana na picha hizo kwani hajawahi kabisa kuwa katika
mazingira hayo na binti huyo bali hao ni mtu ambaye amezitengeneza na
hajui kwanini amefanya hivyo.
Mhe. Komba anasema “Picha nimewahi kupiga nyingi tangu utotoni lakini
hizi za leo hata mimi zinaniogopesha, siwezi kuwa mwaguzi kujua nani
amefanya hivyo lakini ukiangalia kuna roho ya uadui kati yangu mimi na
huyo mtu ambaye ameamua kunifanyizia, kaamua kuingia vitani na anaweza
kufanya hivyo kwa namna nyingi inaweza kuwa kisiasa au kiurafiki lakini
zimenipa tabu sana, zimeisumbua familia yangu, marafiki zangu kwakweli
zimenisumbua sana.”
Mhe. Komba anaendelea kwa kusema kuwa “Nimepokea simu nyingi sana
mpaka nafunga simu kila anayepata anantakia mema, ni wachache
wanaontukana lakini wengine wanantakia mema. Ukiangalia shingo si yangu,
mwili si wangu yule binti mara akae uchi kwahiyo aliyetuma ana sababu
zake na kama kweli mimi ningekuwa nafanya mambo hayo basi angezituma
picha ambazo hata mimi niko uchi kama huyo mwanamke.”
“Mke wangu kanipigia simu kunipa pole , watoto wangu wote ni watu
wazima wamepigia simu kunipa nguvu. Jamii imuogope Mungu mimi namwachia
Mungu apigane na maadui zangu, usifanyie watu usiyotaka kutendewa.”
“Nikijua aliyenifanyia hivyo akija kwa kuniomba msamaha ntamsamehe
lakini hili suala limeniathiri sana kisaikolojia hata bungeni leo
sijaenda.”
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment