Kampuni ya Lifetime ya nchini Marekani imetangaza kipindi kipya cha
Televisheni kitakachoonyesha wazazi vijana wakijifungua porini bila
msaada wa madaktari wakati wa hatua zote za kujifungua lakini pia
hawatakuwa na malazi yoyote katika eneo hilo.
Kipindi hicho “Born in the Wild” kitatoa taswira kwa wanawake na
wanaume ambao wanaamini kuwa kujifunga mtoto katika mazingira mazuri na
kupatiwa huduma zote mbali na madaktari ni njia pekee.
Kipindi hicho kimetokana na video iliyopata umaarufu mkubwa katika
mtandao wa YouTube na kutazamwa mara milioni 20 ikionyesha mwanamke
akijifungua porini lakini tayari wakosoaji wa mambo wanasema kipindi
hicho kinaweza kutoa taswira ya kuhatarisha maisha ya wamama na watoto
wanaopitia mazingira hayo.
Picha hizi zimetolewa na gazeti la Daily mail UK.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment