June 05 2014 mchana kupitia mitandao mbalimbali Tanzania zilisambaa
taarifa zikimuhusu mmiliki wa mojawapo ya nyumba maeneo ya Sakina jijini
Arusha kwamba nyoka aliyekua akimfuga kwa siku nyingi na kuhusishwa na
imani za kishirikina, ameuwawa na Wananchi.
Wananchi
walimuua nyoka huyo na kisha kumkata kata vipande vipande ambapo baada
ya hizi taarifa kusambaa mmiliki wa nyumba hii ameamua kufunguka ili
kutoa maelezo yake ambayo anadai ndio ukweli wenyewe.
Mr.Joseph Paschal Magesa anasema, "Mimi
kama mimi kwanza ni Mkristo safi na mzee wa kanisa na niliondoka
nyumbani jana na mke wangu kutoka Arusha kuelekea Dar es salaam, sijui
lolote kuhusiana na hicho kitu ila nilipofika maeneo ya Mwanga na Same
nikapigiwa simu kwamba kuna nyoka huku ndani ya eneo la garden nyumbani,
kuna vijana niliwaacha wawili pale nyumbani nikawaambia waambieni watu
wawasaidie kumuua huyo nyoka"
"Wakamuita
jirani yangu hapo ndipo naye akanipigia simu nikamwambia bwana wewe si
una bunduki nisaidie kumuua huyo nyoka ila alivyokata simu nilijua
ametekeleza kumbe aliondoka, baadaye napiga tena simu nauliza vipi
naambiwa bado yupo na watu wamejaa nikawauliza kwani hao watu hawawezi
kumuua mpaka bunduki wakasema wanaweza ndio baadae wakanambia wamemvuta
mkia wamemuweka nje ya geti"
"Nikawauliza
anavutika, asije akawa analeta shida wakasema anavutika, nikawaambia
mpelekeni kanisani kwa sababu nyumbani kwangu ni jirani na kanisa ndio
wakamvuta hadi kanisani wakammwagia maji ya baraka kisha wakamkatakata
ndo ikawa mwisho wake hapo".
"Kusema
kwamba nilikua nafuga kwamba huyu nyoka ni mtoto wangu wa kwanza…..
sasa kama ni mtoto wangu wa kwanza si inamaana na mtoto wangu angekufa
na yeye? mimi nasema namwachia Mungu tu…….. sijawahi kusikia Nyoka
kuishi maeneo hayo toka nimeanza kuishi kwa karibu miaka 8, hata na mimi
inanitatiza manake nimetumiwa picha Nyoka amefungwa kitambaa chenye
maandishi mekundu kama ya kiarabuarabu hivi….."
"Taarifa
kwamba Nyoka huyu amevunja kioo cha dirisha akiwa anatokea ndani ya
nyumba, sio kweli…. haipo kabisa hiyo kitu eti kwamba ametokea ndani,
hayo ni mambo ya watu tu… hicho kioo nilikivunja mimi wakati napanga
mizigo ya ofisi yangu… sifahamu chochote kuhusu huyu Nyoka, Watanzania
waniamini haya ninayosema ndio yanayotoka moyoni mwangu"
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment