Katika
historia fupi, Mzee Small alipata elimu ya msingi katika Shule ya
Mingumbi huko Kilwa mkoani Pwani. Mbali na kuwa mkongwe, Mzee Small kila
ulipobahatika kuzungumza naye alikuwa na kawaida ya kutamba kuwa yeye
ndiye msanii wa kwanza kabisa Tanzania Bara kuchekesha runingani.Mzee
Small alianza sanaa hiyo yapata miaka 31 iliyopita na alipata
kufundishwa na mwigizaji Said Seif ‘Unono’ (ambaye pia kwa sasa ni
marehemu).Mbali
na kushiriki sanaa katika vikundi mbalimbali, Mzee Small wakati wa uhai
wake ametumika katika vikundi vya mashirika kama vile Reli, NASACO na
mengine mengi, ambayo kwa sasa hayajihusishi tena na shughuli hizo.Mzee
Small alianza kujulikana sana katika fani ya uchekeshaji hasa pale
alipoibuka na mchezo uliojulikana kama 50, 50, 100, na ule wa Mjini
Shule uliomwelezea mwanamke wa kijijini aliyeolewa mjini.
Mbali
na kutamba na michezo hiyo, Mzee Small alikuwa ni mcheshi na mwenye
kupenda utani wakati wote, aliibuka na kichekesho kisemacho Nani Mwenye
Haki, ambacho baadaye alikiboresha zaidi.
Baadaye
aliibuka na kitu kingine kikali kilichokwenda kwa jina la Nani Kama
Shule, huku akiwa amewashirikisha wakali wengine kama King Majuto,
Kingwendu na wachekeshaji wengine wanaotamba kwa sasa Bongo.
Mzee
Small alikuwa ndiye mmiliki wa kundi la sanaa linalojulikana kama
Afro-Dance ambalo alilisajili mwaka 1994 kwenye Baraza la Sanaa la Taifa
(BASATA) na kutoa ajira kwa vijana wa mitaani.
Pamoja
na kuwa na uzoefu wa kisanaa, lakini mkongwe huyo hakuwahi kuwa na
mpango wa kujiunga na kundi lingine, ila alichokuwa akifanya ni kurekodi
na wasanii wengine alipokuwa akiitwa kwa makubaliano maalum.
Pia
mkali huyo wa vichekesho enzi za uzima wake na uhai wake alikuwa
akijishikiza katika duka moja Kariakoo la Home Shopping Centre
kimatangazo.
Kutokana
na vichekesho, Mzee Small huwa anatania kuwa sanaa ilimpa mke wa ndoa
katika televisheni ambaye ni Bi Chau huku akianisha kuwa mkewe, Bi
Fatuma huwa hana tatizo lolote na Bi Chau kwani anajua kinachoendelea
kuwa ni kazi tu.
MATESO YA KIAFYA
Wakati
akiendelea na harakati za kisanaa, mwaka juzi Mzee Small aliripotiwa
kupatwa na ugonjwa wa kiharusi (stroke) alipokuwa kwenye shughuli za
kisanaa Kanda Ziwa.
Ugonjwa
huo ulimpa mateso makubwa huku akiwa hana msaada wowote. Wakati
akiteseka na kiharusi alipata tatizo linguine kwenye ubongo huku
akitakiwa kila mwezi kwenda kliniki kwa ajili ya ‘check- up.
Hakika
kila nafsi itaonja mauti na leo Mzee Small ambaye mbali na kuiburudisha
alikuwa akitoa mafunzo kwa jamii yetu kupitia kazi zake, leo ameonja
mauti na Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema ampunzishe Mkali huyo wa
vichekesho mahali pema.
-Father Kidevu Blog
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment