Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Jumla ya Ng’ombe  kumi  na Moja  na mbuzi wanne wameuwa  na kuliwa na  mnyama simba   katika   matukio  matatutofauti  yaliyotokea    katika  Tarafa ya  Nsimbo Wilaya ya Mlele  Mkoa wa Katavi  baada ya simba kuvamia katika vijiji vitatu  



 Kwa mujibu wa Diwani wa Kata ya Mtapenda Elieza Fyula  tukio la kwanza  lilitokea  hapo  Mei  28  majira ya usiku  katika Kijiji  cha Kabatini .



 Katika tukio hilo  Simba  walivamia  kwenye kijiji  hicho na kuua na kula  Ng’ombe  watatu  na mbuzi  watano  ambao walikuwa  wako ndani ya zizi la  kufugia mifugo .



 Alisema  siku  iliyofuata ya tarehe 29 meimajira ya usiku  simba hao walivamia  katika  Kitongoji   cha Kambike   kilichoko  katika  Kijiji cha Isinde  na  kuwauwa Ng’ombe  watano  mali ya  mfugaji wa kitongoji hicho aitwaye  Dirisha  na kisha  waliwala ng’ombe hao.



 DiwaniFyula  alieleza  baada  ya tukio hilo  viongozi wa kitongoji walitoa taarifa kwa viongozi wa kata ambao  waliwasiliana na Idara ya Wanyama Poli ambao waliwasili kijijini hapo na kuwaswaga simba hao wapatao watano.



 Alisema siku iliyofuata simba hao walivamia tena kwenye kijiiji cha mkumbi  na kisha waliuwa Ng’ombe wawili na kuwala  


Na  Walter Mguluchuma -Katavi

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top