Polisi nchini Afrika Kusini wanachunguza tukio ambapo
mwanamume mmoja anaripotiwa kumuaa mwanamue mwingine aliyekuwa na
uhusiano na kimapenzi na mwanamuke anayeaminika kuwa mpenzi wake w
zamani.
Alimuua ka kumkatakata vipande na kisha kuula Moyo wake.
Majirani eneo la Malunga lililo
katika mji wa Gugulethu nje ya mji wa Capetown, wanasema kuwa
walikumbana na mwanamume aliyeshuhudia mauaji hayo siku ya Jumanne.
Walioshuhudia wanasema kuwa wakati walipofika
katika mtaa wa kifaharai ambako mshukiwa alikuwa anaishi walimsikia
akisema kuwa "ni yeye mfalme" akisema kuwa bado anampenda mpenzi wake wa
zamani.
Kwa sasa anazuiliwa na polisi
Polisi mmoja aliiambia BBC kuwa wakati
walipowasili eneo la tukio walimpata mshukiwa akila moyo wa binadamu
akitumia uma na kisu.
Walifahamishwa kuwa mwathiriwa alidungwa kisu
upande wake wa kushoto kifuani na kwenye shingo lake na katika sehemu ya
uso alikuwa na alama ya kuumwa.
Marehemu anayeaminika kuwa Bwana Mbuyiselo
Manona,alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamke aliyekuwa mpenzi wa
mshukiwa kwa miaka minne.
Hapakuwa na dalili zozote za mwanamke huyo nyumbani kwake Jumatano lakini gari lake lilikuwa limeegeshwa nyumbani kwake.
Inaripotiwa si mara ya kwanza mwanamke huyo
ambaye anasemekana kuwa na umri wa miaka 50 kuhusishwa na visa
vinavyohusiana na mapenzi. Mumewe aliuawa na mtu anayekisiwa kuwa
mpenziwe mwaka 1996.
Chanzo bbcswahili
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment