UTANGULIZI1. MheshimiwaSpika,kufuatiataarif ailiyowasilishwa hapa
Bungeni na Mwenyekiti wa Kamatiya Kudumu ya Bunge ya Uchumi, Viwanda
naBiashara, naomba kutoa hoja kwamba Bunge lakoTukufu likubali kupokea,
kujadili na kupitishaMakadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya
Fedhakwa mwaka 2014/15.
2. Mheshimiwa Spika, awali ya yote napendakumshukuru Mwenyezi Mungu
mwingi wa rehema kwakuniwezesha kuwasilisha hotuba ya bajeti ya Wizara
yamwaka 2014/15. Aidha, natoa shukrani zangu za dhatikwa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuniteua
kuwa Waziriwa Fedha. Ninaahidi kwamba nitatekeleza jukumu hilikwa weledi
na uadilifu. Vile vile, nawapongeza Mhe.Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) na
Mhe. AdamKighoma Ali Malima (Mb) kwa kuteuliwa kuwa NaibuMawaziri wa
Wizara ya Fedha. Kadhalika, namshukurupia aliyekuwa Naibu Waziri wa
Fedha Mhe. JanethZebedayo Mbene (Mb) kwa utendaji kazi wake mahiri
natunamuombea Mwenyezi Mungu ampe nguvu na afyanjema katika kazi zake
mpya Wizara ya Viwanda naBiashara. Nichukue pia fursa hii kumpongeza
Bw.1Rished M. Bade kwa kuteuliwa kuwa Kamishna Mkuuwa Mamlaka ya Mapato
Tanzania.
3. Mheshimiwa Spika, napenda kukupongeza wewemwenyewe, Naibu Spika
pamoja na Wenyeviti wa Bungekwa kuongoza vyema majadiliano ya Bunge la
Bajeti.
4. Mheshimiwa Spika, naomba nitumie nafasi hiikuishukuru kwa namna ya
pekee Kamati ya Kudumuya Uchumi, Viwanda na Biashara chini ya
Mwenyekitiwake Mhe. Luhaga Joelson Mpina (Mbunge wa Kisesa)na Makamu
wake Mhe. Dunstan Luka Kitandula(Mbunge wa Mkinga) kwa maoni, ushauri
namapendekezo waliyoyatoa kwa Wizara wakati wakuchambua mapendekezo ya
Bajeti ya Wizara ya Fedha.Aidha, nachukua nafasi hii kumshukuru
Mwenyekitiwa Kamati ya Kudumu ya Bajeti Mhe. Andrew JohnChenge (Mbunge
wa Bariadi Magharibi) pamoja naKamati nzima kwa ushauri wao. Katika
uandaaji wahotuba hii, Wizara imezingatia ushauri na mapendekezoya
Kamati hizo pamoja na ushauri na maoni ya hojambalimbali zilizotolewa
wakati wa mjadala wa bajeti yaWizara kwa mwaka 2013/14.
bonyeza hapa juu kusoma hotuba ya waziri wa fedha
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment