Tarehe kama ya leo mwaka jana,msanii wa Hip Hop, Langa Lileo, rais wa gheto mida ya jioni alitangazwa kuwa amefariki dunia,
kwa mujibu wa ripoti ya hospitali msanii huyo alikuwa anasumbuliwa na
malaria kali, alilazwa siku moja katika hospitali ya taifa Muhimbili
siku ya pili yake ndiyo akafariki. Safari ya Langa kimuziki ilianzia
kwenye shindano la kusaka vipaji la Coca-Cola Pop Stars mwaka 2004, na
wakapatikana washindi watatu wakaunda kundi la Wakilisha alikuwemo
Langa, Shaa, na Witness, na ngoma yao ya Hoi.
Langa
alizaliwa Desemba 22, 1985 Jijini Dar Es Salaam alisoma katika shule ya
msingi Olympio na sekondari ya Loyola, pia alisoma Kampala Uganda,
baadaye akapata Stashahada ya masoko katika chuo cha CBE,mkoani Dodoma.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment