Saratani
ya shingo ya kizazi huwa na dalili zake za awali ambazo tutakuja
kuziona. Tunapozungumzia saratani ya kizazi tunalenga zaidi saratani ya
shingo ya uzazi ‘Carcionoma of Cerix’ na saratani ya mfumo wa uzazi au
‘Endometrial Carcinoma.
Saratani
ya mfuko wa kizazi hushambulia zaidi tabaka la ndani la kizazi
‘Endometrium’ na kusababisha maumivu ya tumbo kwa muda mrefu na hata
tumbo kuvimba.
Saratani
hii siyo kubwa sana hivyo hatutaelezea kwa undani ila endapo utakuwa na
maumivu chini ya tumbo na yanasambaa kulia na kushoto na upande wa juu,
tumbo likiwa linaongezeka ukubwa na siku za hedhi zinavurugika, basi
muone daktari wa kinamama kwa uchunguzi wa kina.
Saratani
ya shingo ya uzazi huwapata wanawake walio katika umri wa kuzaa wenye
wapenzi zaidi ya mmoja au ambao mara leo kaolewa na huyu, anaachana naye
anaishi na mwingine, yaani mara kwa mara hana msimamo, anabadilibadili
wanaume, wanawake wanaofanya ngono na wanaume wasiofanyiwa tohara pia
hupatwa na tatizo hili la saratani ya shingo ya uzazi.
Saratani
ya shingo ya uzazi pamoja na kuchangiwa na mambo yote hayo hapo juu,
husababishwa hasa na kirusi kiitwacho ‘Human Papilloma virus’ au kwa
kifupi ‘HPV’. Kirusi hiki huenezwa kwa njia ya ngono, mwanaume huwa
hakimuathiri bali yeye hukibeba na kukisambaza kwa wanawake kwa hiyo
mwanamke anayechanganya wanaume hajui wapi atakipata.
Ukubwa wa tatizo Saratani ya shingo ya kizazi ina tabia ya kusambaa endapo haitagundulika na tiba haitafanyika mapema. Saratani husambaa katika kizazi, nyonga hadi katika mapafu. Ikishambulia nyonga, mwanamke hulalamika maumivu chini ya tumbo.

hii ina tabia ya kusambaa kwa kasi na endapo hatua za haraka
hazitachukuliwa husababisha kifo kwa mwanamke. Saratani huwa
haiambukizi.
Dalili za awali za saratani ya shingo ya uzazi
Mwanamke
mwenye tatizo hili hulalamika maumivu ya tumbo chini ya kitovu, kutokwa
na majimaji yenye harufu ukeni na muwasho mara kwa mara. Tatizo hili
hutibiwa na kujirudia tena mara kwa mara.
Mwanamke
hulalamika kwamba ametibiwa sana kwa dawa za kumeza na kuingia ukeni
lakini hapati nafuu. Hupoteza hamu ya tendo la ndoa, maumivu wakati wa
tendo la ndoa na mwishowe hutokwa na damu ukeni baada ya tendo la ndoa.
Saratani inaposambaa na kushambulia shingo ya uzazi huathiri ukeni na kuumiza njia ya mkojo na kibofu.
Uke
huvimba na kuonekana kuziba na mlango wa kizazi au ngozi ya ndani ya
ukeni ikiguswa tu kidogo basi hutokwa na damu kwani huwa laini sana. Hii
ni hatua mbaya na ya mwisho katika saratani inaposambaa.
Uchunguzi Uchunguzi wa saratani ya shingo ya uzazi hufanyika katika vituo mbalimbali katika kampeni maalum dhidi ya saratani ya shingo ya uzazi.
Uchunguzi Uchunguzi wa saratani ya shingo ya uzazi hufanyika katika vituo mbalimbali katika kampeni maalum dhidi ya saratani ya shingo ya uzazi.
Uchunguzi
pia hufanyika katika hospitali za mikoa na wilaya katika kliniki za
magonjwa ya kinamama ambapo vipimo mbalimbali hufanyika mojawapo ikiwa
ni kuangalia mlango na shingo ya uzazi.
Kipimo
cha Ultrasound pia kitafanyika kuangalia athari katika kizazi. Majimaji
ya ukeni yatapimwa kuangalia maambukizi na uchunguzi wa awali wa
saratani utafanyika.
Endapo mlango wa uzazi utakuwa umeathirika sana, basi kinyama kitatolewa na kupimwa katika maabara kubwa kuthibitisha tatizo.
Ushauri Ni vema mwanamke yeyote anayejihisi maumivu chini ya tumbo na kutokwa na uchafu ukeni na muwasho uwepo au usiwepo awahi hospitali kwa uchunguzi. Waone madaktari wa kinamama kwa uchunguzi sahihi katika hospitali za mikoa.

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment