Ni ukweli usiofichika kwamba kumekuwa na sitofahamu nyingi juu ya wasanii hawa wakali wa Bongo Fleva (Diamond na Alikiba) huku mashabiki wakiwa na kiu ya kutaka siku moja kusikia kazi ya pamoja
iliyofanywa na wakali hao. Hivi karibuni Alikiba ameweka bayana mambo yaliyotokea kati yake na Diamond
Ali Kiba akiwa anahojiwa na kituo kimoja cha redio hapa nchini alifunguka na kusema kuwa, yeye binafsi hana bifu na mtu yeyote hivi sasa, ni mambo tu yaliyowahi kutokea hapo nyuma ambayo hayakuwekwa sawa, alizidi kufunguka na kutoa fumbo kuhusiana na ishu yao na Diamond na kusema kuwa, Unaweza kulinganisha na siku unampa mwanafunzi mwenzako pepa lako kwenye mtihani ili akopi majibu, alafu mwisho wa siku anakuja kukwambia kuwa, pepa lenyewe halifai na kurudishiwa pepa hilo.
Alikiba alisema kuwa kwake yeye hana kinyongo na mtu, ila
kwa lolote lilowahi kutokea Diamond mwenyewe ndio anayetakiwa kuja kumuomba
msamaha Ali kiba ili mambo yaweze kuwa sawa. Mbali na hayo Alikiba alifunguka
na kusema kile kilichokuwa anakifanya wakati akiwa kimya bila kujibu chochote
wakati uvumi na ugomvi huo ukizidi kuongelewa, Alikiba alifunguka na kusema
kuwa alikuwa bize kujifua kwa ujio wake mpya, hasa kwa Project zake anazokuja
nazo upya hivi sasa.
Mbali na kuongelea Ugomvi wao huo baina yake na Diamond, Alikiba alisema kuwa hivi sasa ndio kaja rasmi kuwashika, kaja kuchukua ufalme wake baada ya kutawaliwa kwa muda mrefu sasa kwenye tasnia hii ya Bongo Fleva, Hii sentensi ilikuja na ujio wake mpya wa Kiba Square, kama kundi flani hivi linalojumuisha yeye mwenyewe Ali Kiba na Mdogo mtu, ambao wameweza kutoa wimbo wao hivi karibuni uitwao "Pitambele". Bofya hapa kuisikiliza track hiyo
BONYEZA HAPA
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment