Chelsea wamemsajili kiungo wa zamani wa Arsenal Cesc Fabregas kwa mkataba wa miaka mitano.
Cesc ambaye amekaa miaka mitatu Barcelona, anakwenda Darajani baada ya Arsenal kukataa nafasi ya kwanza ya kumnunua.
Fabregas ambaye yuko Brazil na kikosi cha Spain amesema Chelsea wana mwelekeo anaoutaka na kuongeza kuwa "bado hajamalizana" na Ligi Kuu ya England.
Fabregas ambaye amenunuliwa kwa takriban pauni milioni 27 atavaa jezi namba 4.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment