Mwanamuziki
wa zamani na mbunge Vicky Kamata baada ya ndoa yake kudaiwa kuzuiliwa
kufungwa kutokana na kudaiwa mwanaume aliyetaka kufunga naye ndoa ana
ndoa nyingine, amefunguka kwa kudai kuwa hizo zilikuwa ni habari za
kutungwa na hazikuwa na ukweli wowote.
Vicky
ameiambia amplifaya ya Clouds fm jana kuwa maneno mengi ambayo yalikuwa
yanazungumzwa kuhusu ndoa yake kutofungwa yalikuwa yametengenezwa na
watu.
“Kweli
ni maradhi kama ambavyo ilitangazwa wakati huo, lakini pamoja na hayo
mimi bado nasema mungu alikuwa hajapanga ,alikuwa hajaruhusu kuwa tarehe
24 mwezi wa tano iwe siku wa kufunga ndoa.
“Mimi
kama binadamu na mwenzangu tulipanga lakini mungu alipanga vinginevyo ,
kwaiyo siku zote mapenzi ya mungu huwaga yanatimia siyo mapenzi ya
binadamu.
“Ni
kweli alishawai kufunga ndoa lakini ninachofahamu mimi ni kwamba
waliachana kihalali kabisa kwa divorce ya mahakama ya Kinondoni mwaka
2012 na mimi siyo mtoto mdogo kwamba ninaweza mpaka nikafikia hatua hiyo
bila kuwa nimemchunguza huyo mtu.
“Kuhusu
swala la kwamba alikuwa na mke wake , mke wake alikwenda kuzuia
Kanisani sijui alikuja Bungeni, yale yalikuwa tu ni maneno ambayo
yalitengenezwa na baadhi ya watu kwa interest zao ,lakini siyo kwamba
nilikuwa nimeingilia ndoa ya mtu hata kidogo, kwa sababu ata huyo mke wa
kwanza wa huyo aliyekuwa mchumba wangu aliongea na vyombo vya habari
akasema mimi sijaenda Dodoma wala sijaenda kuzuia harusi.
“Kwaiyo
maneno yaliyokuwa yamezagaa ,sijui mke wake amezuia yalikuwa ni maneno
ya kutengenezwa na watu tu kwa nia zao wenyewe lakini siyo kweli.
“Kuhusu
kwamba hajulikani alipo mimi hilo siwezi kumjibia, mimi nafahamu kwamba
yupo na anaendelea na shughuli zake kama kawaida, kama ambavyo mimi
naendelea na shughuli zangu kama kawaida, tunawasiliana, yani cha
kufahamu tu kwamba ndoa haikufungwa basi.
“Hata
kama kuna mkono wa binadamu katika jambo hilo mimi naamini mungu ndo
mwenye mamlaka na Mungu ndiyo mwenye kupanga mambo, kwaiyo kama Mungu
alikuwa anataka hiyo harusi ifugwe ata kama kungekuwa na binadamu
mwingine hataki bado ingefungwa…
“Kwaiyo
mimi sitaki kuamini sana kwamba kuna waheshimiwa wabunge wenzangu
wamechangia kwa kiasi kikubwa kwamba ndoa ile isifungwe, mimi ninaamini
ni mapenzi ya Mungu tu yametimizwa kwa staili hiyo” Alisema Vicky
CDT: UDAKUSPECIAL
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment