MBUNGE wa
Kawe, Halima Mdee (CHADEMA), amemtaka mbunge mwenzake, Leticia Nyerere,
aache ubunge na akajiunge na Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuliko
kuendelea kukipigia debe chama hicho akiwa upinzani.
Kauli
hiyo ameitoa jana alipokuwa akichangia bajeti ya serikali kwa mwaka
2014/2015 ambapo alisema matendo anayofanya Leticia ya kujipendekeza kwa
CCM yatamgharimu kama ilivyotokea kwa wenzake.
Juzi
wakati akichangia bajeti hiyo, Leticia alisema serikali ikifanya vizuri,
lazima ipongezwe kwakuwa imepeleka maendeleo katika jimbo analotoka.
“Serikali
yangu imefanya mambo mengi, imeniletea maji, walimu katika jimbo langu
la Kwimba, ni lazima tuipongeze si kila wakati tunailaumu humu ndani,”
alisema.
Katika
mchango wake jana, Mdee, alisema jukumu kubwa la upinzani ni kuikosoa
serikali na kuonyesha mbadala katika masuala mbalimbali na si kuisifia
kwa kutekeleza wajibu wake wa kuwahudumia wananchi.
“Serikali
inapata fedha kutokana na kodi za wananchi, inalazimika kupeleka maji,
barabara na huduma mbalimbali kwa lazima si hiyari, tunapoikosoa
tunatimiza wajibu wetu kama yenyewe inavyotekeleza inapowahudumia
wananchi.
“Leticia
Nyerere anaweza kwenda CCM, kwakuwa Rais Kikwete ana nafasi mbili za
uteuzi wa wabunge, lakini lazima ajue waliojipendekeza CCM wamepigika
sana hivi sasa, aachie ubunge aende huko kwakuwa ana mapenzi nao,”
alisema.
Mdee
alisema kuwa Leticia anaiaibisha kambi ya upinzani inayofanya kazi usiku
na mchana kuhakikisha serikali inaboresha huduma inazozitoa kwa
wananchi.
“Upinzani si lelemama, kama anafikiria CCM ni kuzuri zaidi ni vema akaenda huko kuliko kubakia hapa pasipomfaa,” alisema.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment