Na Evance Ng'ingo
Mamia ya
waombolezaji walijitokeza jana katika makaburi ya Kinondoni kumzika
aliewahi kuwa Katibu Mkuu wa klabu ya Yanga, George Mpondela amezikwa
jana katika makaburi ya Kinondoni, Dar es salaam.
MArehemu
Mpondela alifariki dunia ijumaa iliyopita katika hospitali ya Taifa ya
Muhimbili, Dar es salaam alipokuwa amelazwa kwa siku kadhaa kutokana na
ugonjwa wa moyo uliokuwa ukimsumbua. Mpondela aliwahi kuwa Katibu Mkuu
wa Yanga mwaka 1994 na atakumbukwa kutokana na misimamo yake iliyosaidia
kusukuma gurudumu la maendeleo la klabu hiyo kongwe nchini.
Akizungumza
katika maziko hayo Mwenyekiti wa sasa wa Yanga, Yusuph Manji alisema
kuwa Mpondela atakumbukwa kwa mawazo yake yaliyokuwa na mwelekeo chanya
kwa maendeleo ya klabu hiyo. Alisema kuwa marehemu Mpondela alikuwa
akihamasisha uanzishwaji wa Yanga kampuni kwa lengo la kuendeleza zaidi
klabu hiyo.
"Mbali na
kuwa alikuwa Katibu Mkuu muda mrefu uliopita lakini pia alikuja kuwa
mmoja kati ya watu wenye mchango zaidi kwa maendeleo ya klabu hiyo hadi
alipofariki.
"Huyu
hakuwa mtu wa kushindwa kitu alikuwa akipenda kazi yake na alikuwa na
mawazo ambayo ni ya kuendeleza klabu tu aliweza kuiweka klabu pamoja na
wanachama wake pia"alisema Manji.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Wazee wa klabu ya Yanga, Ibrahim Akilimali
alisema kuwa Mpondela aliwatambua na kuwasaidia wazee hao klabuni hapo
hadi alipofariki.
Alisema
kuwa alikuwa akisaidiana na wazee hao katika kusukuma gurudumu la
maendeleo na kuongeza kuwa hakuwa na dharau kwa kila mwanachama.
Katika
makaburi hayo pia walijitokeza watu mbalimbali kumuaga Mpondela akiwamo
Mwenyekiti wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Jamal Malinzi.
credit: matukio na michuzi blog
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment