Msanii wa muziki wa Bongo fleva Dayna
aliye-make headlines na kuzidi ku-hit kwenye tasnia hii ya muziki wa
Bongo fleva, hatimaye afunguka kuhusu picha zilizokuwa zinaleta utata
kwenye mitandao na Blogs mbalimbali nchini, huku ikibua maswali mengi
kuwa wawili hao ni wapenzi au la.”Habari hizo si za kweli, mimi na
Nando ni marafiki tu tulioshibana, na ndio maana tumeweza kupiga picha
zenye ukaribu namna hiyo, kama ilivyo kwa marafiki walioshibana yeye
mara nyingi hunipa kampani, na mimi pia huwa nampa kampani, ila hakuna
mahusiano yoyote ya mapenzi yanayoendelea baina yetu, ni Marafiki tu
toka zamani”- alimalizia kufunguka Dayna, kuweka sawa utata wa picha
alizoweka kwenye mtandao wa instagram na kuzua utata mkubwa.
Post a Comment
Post a Comment