Marekani imeiwekea Uganda
vikwazo kwa kupitisha sheria zinazopinga mapenzi ya jinsi moja katika
taifa hilo la Mashariki ya Afrika.
Afisa wa mahusiano anayesimamia maswala ya
usalama katika ikulu ya whitehouse Caitlin Hayden anasema kupitia kwa
barua kwa wanahabari kuwa sheria hiyo iliyopitishwa na bunge la Uganda
mwezi Februari inakiuka haki za binadamu.
Vikwazo hivyo vitajumuishwa marufuku ya wanaharakati waliopigia debe sheria hiyo kupitishwa kutoingia Marekani.Miradi itakayoathirika na marufuku hiyo ni pamoja na ushirikiano na polisi wa Uganda Wizara ya Afya.
Sheria hiyo inaharamisha uhusiano baina ya watu
wa jinsia moja na wale watakaopatikana wanaweza kuhukumiwa kifungo cha
maisha jela.
Hii ndiyo hatua ya hivi karibuni iliyochukuliwa na Marekani katika ajenda yake ya kupinga sheria hiyo mpya nchini Uganda.Juma lililopita Seneta mmoja kutoka Marekani ,Kirsten Gillibrand alilalmikia vikali uteuzi wa waziri wa maswala ya kigeni wa Uganda Sam Kutesa kuchaguliwa kuwa rais wa Umoja wa Mataifa kutokana na kuwa anatokea Uganda.
Wanaharakati wa wapenzi wa jinsia moja wameenda
mahakamani wakitaka sheria hiyo iondolewe lakini inatarajiwa kupingwa
kwani rais Yoweri Museveni aliupitisha maksudi kudhihirishia wafuasi
wake kuwa yu huru kutokana na shinikizo kutoka kwa mataifa ya ughaibuni .
Punde baada ya kupitishia kwa sheria hiyo mpya
benki kuu ya dunia iliahirisha utoaji wa mkopo wa dola milioni 90 ambazo
zilikuwa zinapaswa kutumika kuimarisha sekta ya Afya nchini Uganda .Mataifa mengi tu ikiwemo Denmark, Norway, Uholanzi na Sweden zote zimekatiza msaada kwa taifa hilo la Afrika Mashariki.
BBC
BONYEZA HAPA
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment