AZAM FC na Yanga zimekutana mara 11 kwenye ligi kuu, Yanga ikiwa imeshinda michezo mitano, huku Azam FC ikishinda michezo minne na michezo miwili zikitoka sare.
Nje ya ligi kuu zimekutana mara tano, Yanga ikishinda mara mbili (Ngao ya Hisani na Kagame Cup na Azam FC ikishinda mara tatu (Mapinduzi Cup na mechi za kirafiki)
Kiujumla Azam FC na Yanga SC zimekutana mara 16 Yanga ikishinda mara saba na Azam FC ikishinda mara saba pia huku michezo miwili timu hizo zikitoka sare.
Tathmini hii inaonesha kuwa timu hizi zina nguvu sawa, yeyote anaweza kushinda mchezo wa leo ambapo timu hizi zinakutana mara ya 17, Je nani atashinda?
John Bocco anaendelea kuwa mchezaji aliyefunga magoli mengi zaidi huku Nadir Haroub Canavaro akiwa mchezaji aliyecheza mechi nyingi zaidi kati ya Azam FC na Yanga.
SOURCE: AZAM WEBSITE
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment