Shabiki mkubwa wa mwanamuziki Justin Bieber aliyekuwa mnene kiasi cha kuwa na kilo 120 amepunguza karibu nusu ya uzito wake ili star huyo kijana aweze kumtambua! notice her.
Akiwa na kilo 67 sasa Bryanna Debinder (20) amepungua kilo 53 kwa mwaka mmoja tu baada ya kuwaonea wivu vi-portable wanaopanda jukwaani ku-show love pindi Justin Bieber anapokuwa anapiga show kwenye matamasha! Na mamuafrica blog
'Kila wakati nikiwaona wasichana warembo wembamba kwa stage huwa natamani ningekuwa mimi' alisema Bryanna. 'Kila mtu anastahili kutambulika kwa mtu anayempenda,mimi ni shabiki mkubwa wa Bieber na nataka kuwa aina ya msichana anayemuimbia'
Wanafunzi wenzake wamesema huwa anatumia muda mwingi kumtumia Bieber ujumbe katika Twitter huku akisikia wivu kuona wasichana wengine wakijibiwa kasoro yeye! Kwa hiyo Bryanna akaachana na vyakula vya mafuta na kupunguza kula
mapochopocho badala yake alijaza friji mboga za majani na matunda.. Pia alikuwa akiangalia video za mazoezi ya mwili You tube huku nae akifanyia kazi na ndani ya miezi 12 alifanikiwa kupunguza uzito wa kilo 53 mwilini! S
Cheki picha za Bryanna kabla na baada ya kupunguza uzito huku akionekana mrembo zaidi.. na nimeamini hakuna linaloshindikana chini ya jua kama ukiamua~!
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment