March 28, 2025 07:25:58 PM Menu
 

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Timu ya taifa ya Ghana imefanikiwa kutinga hatua ya fainali ya michuano ya Afcon baada ya kuwafunga wenyeji Equatorial Guinea katika mchezo wa nusu fainali uliopigwa usiku wa kuamkia leo.
Ghana wakiingia kwa kujiamini baada ya kuwatoa Guinea katika hatua ya robo fainali walianza kuonyesha dhamira yao mapema wakishambulia lango la wapinzani wao kwa nguvu na walipata bao mapema kwenye dakika 42 mfungaji akiwa Jordan Ayew ambaye alifunga kwa mkwaju wa penati baada ya kipa wa Equatorial Guinea kumchezea vibaya Kwesi Appiah.
Ghana walifunga bao la pili kupitia kwa Mubarak Wakaso  ambaye alifunga kwenye dakika ya 46 baada ya kupokea pasi toka kwa Christian Atsu .
Nahodha wa timu hiyo katika mchezo huo Andre Ayew ambaye alikuwa anshikilia nafasi ya Asamoah Gyan alifunga bao la tatu kwenye dakika ya 75 na kuua matumaini ya Equatorial Guinea kucheza fainali .
Mchezo huo ulilazimika kusimama kwa muda baada ya mashabiki wa Equatoarial Guinea kuanza kufanya vurugu wakionyesha hasira zao baada ya kufungwa .
Ghana ambao wameingia kwenye fainali yao ya kwanza tangu mwaka 2010 watakutana na Ivory Coast katika mchezo wa fainali utakaopigwa jumapili ijayo huku Equatorial Guinea wakicheza mchezo wa kuwania nafasi ya tatu dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo siku ya jumamosi.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro
06 Feb 2015

Post a Comment

 
Top