March 15, 2025 08:44:27 PM Menu
 

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Mshambuliaji aliyejiunga na Barcelona akitokea Liverpool msimu uliopita Luis Suarez amekumbushia cheche zake nchini England kwa kuiongoza timu yake ya sasa ya Barcelona kuikaanga Manchester City kwa kuichapa mabao 2-1 Katika mchezo wa hatua ya 16 bora ya Kombe la Mabingwa barani Ulaya.
Katika mchezo huu uliopigwa Etihad Stadium, Barcelona wameanza kujipatia mabao yao katika dakika ya 16 na 30 kupitia kwa Luis Suarez ‘Mnyama’ na wenyeji Manchester City wamepata bao lao kupitia kwa Sergio Aguero dakika ya 69 huku Gael Clichy akitolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 74 baada ya kupata kadi ya njano ya pili.
Katika dakika za majeruhi, Lionel Messi amekosa penati iliyochezwa kwa ustadi na kipa wa City Joe Hart, penati iliyopatikana baada ya Zabaleta kumchezea vibaya Messi katika eneo la hatari
Timu hizi zitarudiana Machi 18, 2015 katika dimba la Camp Nou nchini Hispania.
Timu hizi pia zilikutana katika msimu uliopita katika hatua kama hii na Barcelona kuitupa nje Manchester City kwa jumla ya mabao 4-1.
Je, uonavyo wewe historia hii itajirudia?
Mechi nyingine imepigwa Juventus Stadium Turin nchini Italia kati ya Juventus na Borrusia Dortmund na kushuhudia Juventus ikiichapa Borussia Dortmund mabao 2-1.
Marudio ya mechi hii pia ni Machi 18 katika dimba la BVB Stadion Dortmund nchini Ujerumani

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro
25 Feb 2015

Post a Comment

 
Top