
Mechi ya Ligi Kuu iliyopigwa usiku huu kati ya Azam FC na Tanzania Prisons katika uwanja wa Azam Complex Chamazi imemalizika kwa matokea ya suluhu ya bila kufungana.
Kwa matokeo haya Azam imefikisha point 27, ikiwa ni point 4 nyuma ya Yanga ambayo inazidi kujitawala kileleni ikiwa na point 31.

Prisons imefikisha point 12 ikiwa mkiani mwa msimamo wa ligi
Awali katika uwanja huo ulipigwa mchezo wa fainali wa Ligi Daraja la Kwanza FDL kati ya Mwadui ya Shinyanga na African Sports ya Tanga na kushuhudia Mwadui wakiibuka machampion baada ya kuifunga African Sports bao 1-0 na kukabidhiwa kombe la Ligi Daraja la Kwanza msimu wa 2014/15
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment