Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Majogoo wa Liverpool leo wameonesha makucha yao katika mchezo wa ligi kuu ya England baada ya kuichapa timu ngumu ya Southampton mabao 2-0.
Mabao ya Liverpool yamefungwa na Philippe Coutinho dakika ya 3 na Raheem Sterling dakika 73.

Matokeo hayo yameifanya Liverpool ipande hadi nafasi ya 6 baada ya kufikisha point 45 nyuma ya Southampton yenye point 46 na kuiacha Tottenham Hotspur nafasi ya 7 ikiwa na point 44.
Katika nafasi ya 4 ipo Manchester United yenye point 47 na Arsenal inashika nafasi 3 ikiwa na point 48.
Katika mechi nyingine za leo katika ligi hiyo ni
Tottenham Hotspur 2 - 2 West Ham United
Everton 2 - 2 Leicester City
Southampton 0 - 2 Liverpool

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro
22 Feb 2015

Post a Comment

 
Top