March 16, 2025 08:03:44 PM Menu
 

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Na Laurent Samatta
MCHEZA filamu za Kibongo Jennifer Kyaka ‘Odama’, amedai kuwa mwanaume ambaye anaweza kumuoa jambo la kwanza lazima atambue kuwa yeye anafanya filamu kwa muda mrefu hivyo hawezi kuacha kazi yake kwa sababu ya kuingia kwenye ndoa.

Mcheza filamu za Kibongo Jennifer Kyaka ‘Odama’.
Odama alifungua kinywa chake baada ya kuzungumza na paparazi wetu, ambapo alidai kuwa haiwezi kutokea kuacha kufanya filamu ili amridhishe mwanaume kwani maisha yake yamekuwa yakiendeshwa na kazi hiyo kwa muda mrefu.
“Naamini kuwa yule ambaye atakuja kwa nia ya kunioa kwanza lazima atambue kuwa nafanya filamu, sitahitaji anieleze jambo la kuacha kazi yangu, mimi ni mwanamke ambaye nahitaji kupata maendeleo kupitia kazi zangu,” alisema.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro
08 Jan 2015

Post a Comment

 
Top