STORI: Musa Mateja
MCHUMBA wa Video Queen maarufu Bongo, Agnes Gerald ‘Masogange’ aitwaye Evance Kom juzikati alijikuta akivunja ukimya kwa kuweka wazi kuwa msichana huyo amemsaliti baada ya kuvunja makubaliano yao.
MCHUMBA wa Video Queen maarufu Bongo, Agnes Gerald ‘Masogange’ aitwaye Evance Kom juzikati alijikuta akivunja ukimya kwa kuweka wazi kuwa msichana huyo amemsaliti baada ya kuvunja makubaliano yao.
Akizungumza na gazeti hili Jumatatu hii, alisema hana tena mpango wa
kuoana na Agnes kwani kitendo chake cha kuamua kuhamia Afrika Kusini
kimeonyesha wazi hawawezi kuishi tena pamoja.Akisimulia, Evance alisema
hapo awali walikubaliana kuwa pamoja kiasi kwamba hadi kufikia
kumvalisha pete, wazazi wa pande zote mbili walikwishajua na kubariki
uhusiano wao.
“Wakati anapanga mipango yake ya kuhamia Afrika Kusini, hakuwahi
kuniambia hata mara moja, alikuja kuniambia eti tuhamie huko siku chache
tu kabla hajaondoka, nisingeweza kuondoka na kwenda kuanza maisha mapya
huko wakati hapa Bongo nina miradi yangu kibao,” alisema.
Alisema kutokana na kitendo hicho cha kuhamia huko, pia mchumba wake
huyo alikuwa amejiingiza kwenye mambo yasiyofaa ambayo wazazi wake
wasingeweza tena kumsapoti kama angehitaji kuendelea na nia yake ya
kumuoa.
“Nilimpenda sana Agnes na yeye alinipenda lakini alichokiamua ni
kizuri kwake, ila kwangu ni kama amenisaliti maana kajiingiza kwenye
mambo yasiyofaa hivyo kwa sasa amebaki kama rafiki yangu wa kawaida tu,”
alisema.
Chanzo Global
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment