Stori: Hami da Hassan na Haruni Sanchawa
KIFO
cha tajiri maarufu mjini Bukoba, Leonard Mtensa (50) ambacho
kimetingisha kanda nzima ya ziwa, kilichotokea dakika chache baada ya
marehemu kudaiwa kufanya mapenzi ndani ya gari lake, sasa mambo
hadharani juu ya kila kitu kilichotokea, Risasi Jumamosi linakupa mkanda
mzima.
Tajiri maarufu mjini Bukoba, Leonard Mtensa akichunguzwa na daktari.
Tukio hilo lililozua gumzo mjini Bukoba, lilitokea usiku Novemba 18,
mwaka huu ambapo imeelezwa kuwa marehemu ambaye ni baba wa familia,
kabla ya kupatwa na umauti, alikutwa ndani ya gari yake aina ya IST
lenye namba za usajili T. 982 CQG akifanya mapenzi na mchepuko wake
aliyetajwa kwa jina la Jackline Hassan (25) maeneo ya Buyekere mjini
Bukoba.
Mwili wa marehemu, Leonard Mtensa ukitolewa hospitali ya mkoa wa Bukoba kupelekwa nyumbani kwake kuzikwa siku ya leo.
TUJIUNGE NA CHANZO
Kwa mujibu wa chanzo makini,
siku ya tukio marehemu ambaye anamiliki Klabu ya Linas, alidaiwa kunywa
pombe kali aina ya Whisky Bond pasipo kula vizuri huku akisumbuliwa na
tatizo la presha hivyo wakati akifanya yake ndani ya gari, ghafla presha
ilipanda, akaanza kutapatapa.
Msafara wa magari ukitoka kuchukua mwili wa marehemu hospitali kuelekea nyumbani kwake.
“Si unajua tena jamaa umri umeenda kidogo
na anasumbuliwa na presha, sasa inawezekana na kinywaji alichokunywa
ndiyo kilitibua zaidi. Pombe ukiwa hujala huku una tatizo la presha
madhara yake ndiyo haya,” kilisema chanzo chetu.
Mke wa marehemu akiwa haamini kama mumewe amefariki.
APEWA MSAADA
Baada ya hali yake kubadilika
ghafla, inadaiwa kuwa mpenzi wake badala ya kukimbia kama ambavyo
wengine hufanya, yeye alifanya juhudi kubwa kujaribu kuokoa jahazi kwa
kupiga simu kwa marafiki wa marehemu, lakini kabla hawajafika, mtu mmoja
alitokea na kumsaidia marehemu kumpeleka katika kituo cha Afya cha
CLCT-Ndolage.
AFIA NJIANI
Chanzo hicho kilizidi kumwaga data
kuwa, baada ya mtu huyo kujitolea kumkimbiza hospitali, hali ya Mtensa
ilizidi kuwa mbaya ambapo alifariki kabla hajafika hospitali.
“Wakati wanamchukua kwenye gari, mapigo ya moyo yalikuwa yakimwenda mbio
sana kabla hajafika hospitali akafariki,” kilisema chanzo chetu.
Binti aliyekuwa na marehemu.
HOFU KWA MREMBO
Chanzo kilidai kuwa, baadhi ya
marafiki wa marehemu waliingiwa hofu na mrembo huyo na kuwa na wasiwasi
wakihoji chinichini kwamba pengine alimpa marehemu kitu kibaya.
“Marafiki wa marehemu waliingiwa hofu sana na mazingira ya kifo,
walikuwa wakijiuliza isije kuwa mrembo aliyekuwa naye amempa kitu chenye
madhara,” kilisema chanzo chetu.
ASHIKILIWA NA POLISI
Kamanda wa polisi mkoa wa Kagera, ACP Henry Mwaibambe alikiri kutokea
kwa tukio hilo ambapo alisema wanamshikilia Jackline kwa ajili ya
upelelezi zaidi.
Waombolezaji wakiwa nyumbani kwa marehemu.
AIBU, SIMANZI MSIBANI
Chanzo hicho kilizidi
kueleza kuwa, msibani nyumbani kwa marehemu maeneo ya Kyakairabwa, kata
ya Nyanga, waombolezaji walikuwa wakiona aibu kuzungumzia kifo chake
hadharani kwa kuona ni kashfa hasa kwa kuwa marehemu alikuwa mtu
anayeheshimika katika jamii.
Jeneza la marehemu, Leonard Mtensa.
“Unajua hakuna mtu hata mmoja ambaye anataka kuongelea kifo cha baba
huyo, hata marafiki zake hawaongei kabisa kwani wanaona kuwa ni kashfa
kwa sababu Mtensa alikuwa ni mtu maarufu sana si kwa hapa Bukoba tu,
bali hata jijini Mwanza na kanda ya ziwa kwa jumla,” kilisema chanzo
hicho.
WHISKY BOND IPOJE?
Ili kutaka kufahamu uhusiano wa kilevi alichokutwa nacho marehemu na
kifo chake, Risasi Jumamosi lilimtafuta daktari mmoja mtaalamu wa
magonjwa ya binadamu, (jina linahifadhiwa) ambaye alisema kitendo cha
mwanaume kupoteza maisha akiwa anafanya mapenzi ni jambo la kawaida.
“Wako watu wanaofariki wakiwa wanafanya tendo, inategemea, wengine
wanakuwa na historia ya magonjwa kama shinikizo la damu, sasa ile nguvu
inayotumika katika tendo na kama ugonjwa utatokeza wakati huo, uwezekano
wa kupoteza maisha ni mkubwa.
“Halafu pombe kama hii ni kali, sasa kama mtu alikuwa na matatizo ya
presha, akawa amezidisha kiwango ni rahisi zaidi ku-collapse (hali
kubadilika) wakati wa tendo. Tatizo lingine linaweza kuwa ni aina ya
vyakula anavyokula kufuatia matumizi ya pombe yenye kilevi cha juu.
Mfano wa gari aina ya IST alipokutwa marehemu.
“Maana unakuta mtu mwingine anakunywa kilevi kikali lakini hapendi
kula, hili nalo ni tatizo kubwa. Vinywaji vikali mara nyingi vinaendana
na ulaji wa vyakula vyenye mafuta kwa sababu hivi huenda kukausha damu,”
alisema.Marehemu aliyeacha mjane na watoto, alitarajiwa kuzikwa jana
mjini humo.
Chanzo Global
Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi
Post a Comment
Post a Comment