Machafuko yaliyotokea nchini Burkina Faso yamepelekea Rais wa nchi hiyo kutangaza kujiuzulu na nchi kubakia ikiongozwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Honore Nabere Traore.
Rais aliyejiuzuru Blaise Compaore amesema amechukua maamuzi hayo ili kuiruhusu hali ya amani iweze kurejea baada ya kuzuka machafuko mitaani watu wakipinga kitendo cha bunge kutaka kufanya mabadiliko ya katiba ili imruhusu Compaore aendelee kukaa madarakani.

Compaore amekaa madarakani kwa miaka 27.
Machafuko yalipelekea uharibifu mkubwa ikiwemo jengo la Bunge kuchomwa moto, na safari za ndege kusitishwa katika uwanja wa ndege wa Ouagadougou.
Bonyeza Hapa kuungana nasi facebook
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro








Post a Comment
Post a Comment