Wapiganaji wa Boko Haram Taarifa kutoka Kaskazini Mashariki mwa Nigeria zinasema kuwa zaidi ya wanawake 60 wakiwemo wasichana wa umri mdogo waliotekwa nyara mwezi jana na Boko Haram wamekwepa.Taarifa hii inakuja wakati sawa na taarifa za kutokea makabiliano makali kati ya jeshi la Nigeria na wapiganaji wa kundi hilo.
Serikali
ya Nigeria imeitisha uchunguzi wa kina juu ya namna walivyotoweka
wasichana hao.Wanawake hao wanaaminiwa kuwa miongoni mwa wanawake 68
waliotekwa nyara mwezi uliopita karibu na mji wa Damboa Kaskazni
Mashariki mwa jimbo la Borno.Hali ya usama ni mbaya sana huku miundo
mbinu duni ikichangia kuifanya hali ngumu kuweza kufikia maficho ya
kundi hilo na pia kubaini idadi ya wasichana waliotoroka kutoka mikononi
mwa Boko Haram.
BBC imeongea na jamaa ya wasichana watatu ambao walitoroka. Sasa wako
salama nyumbani kwao na mmoja wao amesema kwamba wasichana wengi
wamefanikiwa kutoroka.
Baadhi ya
vyombo vya habari nchini humo vinadai kuwa huenda wasichana hao
walitoroka siku ya Ijumaa, pale watekaji nyara walipokwenda kushamblia
kambi ya kijeshi.
Maafisa wakuu hata hivyo bado hawajaweza kuthibitisha kukwepa kwa wasichana hao.
Wakati huohuo hapajakuwa na taarifa zozote kuhusu wasichana 200 waliotekwa nyara katika shule ye mabweni ya Chibok mwezi Aprili.
Hatua ambayo
imekemewa vikali na jamii ya kimataifa huku baadhi ya mataifa kama vile
Marekani, Uingereza na hata Ufaransa wakijitolea kuisaidia serikali ya
Nigeria kuwasaka wasichana hao.
CHANZO: bbc
UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WHATSAPP 0712-483 331
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu BONYEZA HAPA
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment