WANANCHI
wanaoishi Mivinjeni Kurasini katika Wilaya ya Temeke jijini Dar es
Salaam wameandamana na kufunga barabara ya Kilwa kwa muda wa zaidi ya
masaa Matatu, wakiwa na mabango yenye ujumbe wa malalamiko ya kudai
kulipwa fidia zao ili kupisha mradi wa ujenzi wa bandari kavu kwenye
eneo hilo. Mashuhuda wa tukio hilo amesema kuwa wamefikia uamuzi huo kwa
lengo la kuitaka Serikali kuwalipa fidia ya fedha za nyumba zao
zilizowekewa alama na serikali kwa ajili ya kubomolewa na kupisha mradi
wa ujenzi huo. Shuhuda amesema vurugu hizo zimepelekea baadhi ya
wananchi kujeruhiwa kwa kupigwa mabomu ya kutoa machozi pamoja na
virungu, zoezi lililofanywa na Askari wa Kikosi cha kutuliza ghasia
(FFU). Wakazi hao wamesema kuwa Serikali ilikubaliana na
mwekezaji kuwalipa pesa zao na kutafutiwa viwanja huko Kibada lakini
cha kusikitisha zoezi la ulipaji hundi lilisitishwa hapo jana mpaka
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Tibaijuka
atakapotoa tamko lini walipwe. Aidha, katika tukio hilo baadhi ya magari
yaliyokuwa yanatumia barabara hiyo yalizuiwa kupita na wananchi hao kwa
kuweka mawe barabarani na matairi ya magari wakitaka kuyachoma kwa
lengo la kuzuia shughuli zozote kutoendelea katika eneo hilo. Kwa mujibu
wa ITV, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadik akiongea kwa
njia ya simu amemuagiza Mkuu wa Wilaya kuhakikisha watu hao wanatawanywa
na yeyote atakayekaidi achukuliwe hatua za kisheria kwani si taratibu
sahihi kufunga barabara na kusababisha usumbufu kwa watumiaji barabara
ambao hawahusiki. Chanzo;Fikra Pevu
UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WHATSAPP 0712-483 331
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu BONYEZA HAPA
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment