SAKATA
la wafanyakazi wa ndani kunyanyaswa na mabosi wao limeingia katika
sura ya kipekee, safari hii mabosi wamegeukwa ambapo mmoja amedaiwa
kuuawa na hausigeli wake aliyetajwa kwa jina la Valentina Karenge (17).
Hatua
hiyo imekuja siku chache baada ya mfanyakazi huyo wa ndani mkoani
Singida kudaiwa kumuuua tajiri yake kwa kumchoma kisu sehemu ya juu ya
titi la kulia kwa madai ya kunyanyaswa naye. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida (SACP) Geoffrey Kamwela alisema tukio hilo la aina yake lilijiri saa 10 alfajiri Juni 29, mwaka huu eneo la Sabasaba, Kata ya Utemini, Manispaa ya Singida. Kamanda Kamwela alimtaja marehemu kuwa ni Pendo Justine Kiula (24) ambaye ni Karani wa Mahakama ya Wilaya ya Singida.
Ndugu,jamaa na marafiki wakitoa heshima za mwisho kwa marehemu, Pendo Justine Kiula.
“Baada
ya marehemu kuchomwa kisu na msichana wake huyo, alitoka nje ya nyumba
na kukimbilia kwa majirani kwa ajili ya kuomba msaada lakini wakati
majirani wakiwa katika harakati za kumpeleka hospitali, alianguka chini
na kufa papo hapo,” alisema Kamanda Kamwela. Alisema baada ya polisi kuendesha msako kwa kushirikiana na raia wema hatimaye walifanikiwa kumkamata msichana huyo majira ya saa 8 mchana uliofuata maeneo ya Uwanja wa Ndege akiwa katika harakati za kutoroka.
.....wakiendelea kuaga mwili wa marehemu.
Naye
Naomi Abrahaman ambaye ni mpangaji mwenzake marehemu, alisema kabla ya
tukio hilo walikuwa pamoja jioni na kushiriki chakula cha jioni na
kisha wakaenda kulala.Alisema ilipofika saa kumi kasoro usiku, alishituka kugongewa mlango na marehemu na alichokisikia akikizungumza ni; Kwa jina la Yesu nakufa, kwa jina la Yesu nakufa.’
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida (SACP) Geoffrey Kamwela akitoa ufafanuzi kuhusu kesi hiyo ya mauaji.
“Alipiga
mlango wangu kwa nguvu na damu zilikuwa zikimvuja, akaenda kwenye
chumba kingine cha mpangaji akapiga tena mlango huku akisema jamani
nisaidieni nakufa, kwa jina la Yesu nakufa, akaanguka.
“Nilipotoka
chumbani, nilimkuta ameanguka chini huku akiwa ameshikilia pale
alipochomwa kisu huku damu zikiendelea kumtoka.” Alisema mpangaji huyo.
Mungu ailaze mahali pema peponi roho yake. Amina.
Huu ni mfano wa kisu kilichotumika katika mauaji hayo.
Akaendelea:
“Kumbe mtuhumiwa alimchoma kisu wakati chumb ani kukiwa na giza,
baada ya kufanya tukio hilo alikimbia nasi tukawa tunaogopa kuingia
chumbani kwa kuhofia pengine kunaweza kukawepo mtu aliyejibanza ndani
ya chumba hicho.”
Marehemu alizikwa Julai 2, mkoani Singida. Ameacha mtoto mmoja. Mungu ailaze mahali pema peponi roho yake. Amina.
Credit GPL
UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WHATSAPP 0712-483 331
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu BONYEZA HAPA
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment