Mchezaji nguli wa Real Madrid Alfredo Di Stefano, anayetajwa kuwa mmoja wa wachezaji wazuri duniani amefariki dunia.
Mchezaji
huyo wa zamani wa Real Madrid aliyekuwa na umri wa miaka 88 alipatwa na
mshtuko wa moyo siku ya Jumamosi na kulazwa katika hospitali ya
Gregorio Maranon mjini Madrid.
Real
Madrid imethibitisha taarifa hizo, ikisema Di Stefano ambaye ni Rais
wao wa heshima amefariki dunia.Katika uhai wake alishinda makombe matano
ya Ulaya,
akifunga katika kila mchezo wa fainali kati ya mwaka 1956 na 1960.Rais
wa Real Madrid, Florentino Perez amesema bodi ya klabu 'imesikitishwa na
kupeleka rambirambi kwa watoto, familia na marafiki'.
Alizaliwa
nchini Argentina, lakini mafanikio yake aliyapata Ulaya kwa kuweza
kushinda vikombe vinane vya ligi kuu ya Spain, na kuwa mchezaji bora wa
mwaka wa Ulaya mwaka 1957 na 1959.
UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WHATSAPP 0712-483 331
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu BONYEZA HAPA
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment