Ingawa Diamond hayupo
Tanzania lakini hakungoja mpaka arudi ndipo akabidhi zawadi hii badala
yake alichokifanya ni mara baada ya kukamilisha kila kitu kinachoihusu
gari hii Diamond Platnumz aliwapatia mameneja wake kwa ajili ya
kuiwasilisha kwa mama yake.
Ni Toyota Lexus New Model ambapo Babu Tale amesema imegaharimi milioni 38.1 ambapomilioni
35 imetumika kulinunulia gari hilo mpaka kuingia Tanzania na Milion 3.1
imetumika kulipamba na kuweka Music System pamoja na seat Cover.
Zawadi
hii ameitoa Diamond kwa mama yake kama zawadi kwa ajili ya kuadhimisha
siku yake ya kuzaliwa kwa mama yake ambaye amesema ametimiza miaka 55,
mama yake amesema hakutegemea zawadi hii na anamuombea mwanae kwa Mungu
afanikiwe zaidi.
Baada
ya kufuturu Meneja wa Diamond Babu Tale alitangaza utaratibu wa
kuzindua kwanza video mbili za Diamond kwa watu waliokuwepo hapo kisha
utaratibu mwingine ukaendelea ikiwemo kumuimbia mama yake Diamond kisha
kukabidhiwa gari yake
UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WHATSAPP 0712-483 331
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu BONYEZA HAPA
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment