Mtu aliyekuwa amevaa bomu kwa siri amemuua ndugu wa rais wa Afghanistan, Hamid Karzai kusini mwa jiji la Kandahar.

Maafisa
wameelezaa kuwa Hashmat Karzai alikuwa anapokea wageni katika nyumba
yake walioleta salam za Eid, ndipo mtu huyo alipojilipua na kumuua yeye
pia.
Ndugu
huyo wa rais Hamid anayefahamika kwa jina la Hashmat Karzai alikuwa
meneja kampeni wa Ashraf Ghani ambaye ni mmoja kati wagombea wawili wa
urais wanaopewa nafasi kubwa ya kukikalia kiti cha Hamid Karzai baada ya
uchaguzi.

Hakuna kundi lolote lilidai kuhusika na mauaji hayo.
Kundi la Taliba limekuwa likijihusisha na mauaji katika jiji hilo wakati ambapo wakielekea kwenye uchaguzi wa rais.
UKIONA TUKIO LOLOTE LINATOKEA USISITE KUTUTUMIA PICHA KUPITIA WHATSAPP 0712-483 331
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu bonyza hapa
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment