Mvua
kubwa iliyoambatana na radi na upepo mkali imesababisha mafuriko
yaliyoharibu barabara na nyumba hivyo kulazimisha baadhi ya familia
zinazoishi maeneo ya mabondeni kuhama huku nyingine zikipoteza mali zao.
Mwananchi
lilifika katika baadhi ya maeneo na kushuhudia familia zikiwa nje ya
nyumba zao na wengine wakiwa wamefungia vitu vyao ndani na kuelekea
maeneo mengine wakisubiri maji yakauke ili warejee katika nyumba zao.
Samani
kama magodoro, makochi na vitanda vilionekana vikiwa vimetolewa nje
kutokana na maji kujaa ndani ya nyumba hizo, ishara kwamba maisha
hayaendi sawa kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.
Katika
eneo la Jangwani, kuanzia ulipo ukingo wa Mto Msimbazi mpaka katika
sehemu ya eneo la makao makuu ya timu ya Yanga, maji yamejaa kiasi cha
kuvuka magoti ya mtu mzima.
Eneo
hilo limefurika na wananchi waliohojiwa wamesema kuwa, sababu kuu ni
kuzibwa kwa mfereji unaopeleka maji baharini katika Barabara ya Morogoro
kutokana na ujenzi unaoendelea kwenye barabara hiyo.
Ally
Mgoha (95) mkazi wa Jangwani alisema endapo mfereji unaopitisha maji
ungezibuliwa basi adha hii waipatayo ingepungua kwani hivi sasa hali si
nzuri katika eneo hilo.
“Wananchi
tumechanga pesa ili mfereji uzibuliwe lakini tulinyimwa kibali kutoka
kwa ‘wakubwa’. Sisi hatuwezi kuhama hapa kwa sababu ni kwetu na
tumejenga tangu kwa kipindi kirefu…watu wametumia mamilioni ya fedha
kujenga nyumba zao,” alieleza Mgoha.
Mgoha
anasisitiza kuwa hata waliokwenda Mabwepande wanarudi kutokana na
kuchoshwa kuishi katika mahema baada ya ahadi ya Serikali kuwapa vifaa
vya ujenzi kutotekelezwa.
“Mwanangu mmoja yupo kule lakini shida azipatazo ni nyingi,
Mwananchi
lilifika katika Ofisi za Serikali za Mitaa ya Mtambani ‘A’ na
kushuhudia ofisi hizo nazo zikiwa zimefurika maji na baadhi ya nyaraka
zilizolowa zikianikwa huku juhudi za kuyatoa maji nje ya ofisi hizo
zikiendelea.
Mwenyekiti
wa mtaa huo, Ally Hamed alisema fedha zilizochangwa na wananchi
hazitoshi kukodi vifaa vya kuzibua mfereji ili kupunguza adha waipatayo
wakazi wa eneo hilo.
Katika
maeneo ya Chang’ombe makaburini, Mwananchi lilishuhudia baadhi ya
makaburi yakiwa yamezingirwa na maji na hata mboga zinazolimwa katika
eneo hilo zikiwa zimefunikwa na maji.
Baadhi ya wakulima waliokutwa eneo hilo walieleza kuwa mvua imewasababishia hasara kwa kuwa mazao yao hayawezi kustawi tena kama walivyotarajia.
Chanzo;Mwananchi
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro







Post a Comment
Post a Comment