HAUSIGELI
aitwaye Melina Mathayo mwenye umri kati ya miaka 15, ameumizwa vibaya
sehemu za kichwani na kulazwa katika Hospitali ya Mwananyamala jijini
Dar es Salaam baada ya kupigwa na bosi wake aitwaye Yasintha Rwechungura
mkazi wa Boko.Majeraha aliyonayo kichwani Melina Mathayo baada ya kupigwa na bosi wake.
Akiongea
na mwanahabari wetu akiwa katika hospitali hiyo, Melina amesema amekuwa
akipigwa na bosi wake huyo mara kwa mara kwa kutumia waya, brenda na
vifaa vingine japo alikuwa akiogopa kusema.
Vitendo
hivi vya ukatili vinaonekana kushamiri kwa sasa ikiwa ni siku chache
baada ya hausigeli aitwaye Yusta kuripotiwa kung'atwa na bosi wake
aitwaye Amina Maige aliyepandishwa kizimbani leo katika Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kinondoni.
Binti
huyo aliyeletwa Mwananyamala leo alfajiri akiwa na hali mbaya amefanya
kazi kwa miaka miwili nyumbani kwa mama huyo mwenyeji wa mkoani Kagera.
Melina
alikuwa akiongea na mwanahanbari wetu akiwa na mpira wa kuongezewa damu
mwilini na amehamishiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu
zaidi.
Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mwananyamala amethibitisha kutokea tukio hilo.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment